Home Education Exams KCSE Kiswahili Paper 2 2017 PDF: Free Past Papers

KCSE Kiswahili Paper 2 2017 PDF: Free Past Papers

0
SHARE

KCSE Kiswahili Paper 2 2017 PDF -- If You are among the Candidates that will be writing Kiswahili in the upcoming KCSE exams this year, review the past paper 2, It is very helpful. After a successful download of the PDF of KCSE Kiswahili Past Paper 2 for 2017, and start practicing the KCSE Kiswahili Paper 2 2017 consistently You will see good results.

KCSE Kiswahili Paper 2 2017

What to expect: kcse Kiswahili past papers 2017, KCSE Kiswahili Paper 1 2017, kcse Kiswahili 2017 questions and answers, kcse Kiswahili topics, KCSE Kiswahili Paper 2 2017 and more

The KCSE Kiswahili past Papers with answers will prepare You for the upcoming KCSE exams 2020, We believe that past questions are worth It when it comes to revision for KCSE examinations. You must know that there are no new questions, it’s just a repetition of already-set questions but in a different tricky form.

KCSE Kiswahili PAPER 2 2017 WITH ANSWERS

If You decide to buy the past revision Papers from us, the content of What You will receive for every order are as follows

We will send the KCSE Kiswahili Past Papers PDF to your email for You to download and study. But If You download the free version on this page, certainly the marking schemes may be limited and obviously the KCSE prediction questions are not attached.

If You have any problems or enquires about KCSE Kiswahili Paper 2 2017, please visit portal.starbinet.com to post your questions and answers.

You can as well leave a comment below and We will respond accordingly.

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili Past Paper 2

KCSE Kiswahili Paper 2 2017 Questions and Answers
KCSE Past Papers 2017 Kiswahili and Government Paper 2

2017 Kiswahili Karatasi ya 2

Lugha

UFAHAMU: (Alama 15)

Soma kifimgu kifilatacho kisha ujibu maswali.

“Asante baba, asante mama,” akasema Bahati jioni moja baada ya chajio, “Sijui ilitokeaje kukawa na Waru Wanaothamini binadamu Wenye mahitaji maalumu katika jamii hii. Sitawauliza mlichofanya kunikinga na hukumu ya ukoo ya kuniangamiza; hayo mtakuja kunihadithia siku rnoja. Ila nataka rnjue kwamba khishi na ulemavu Wa aina yoyote ile kuna dhiki kuu. Niliyokabiliana nayo baada ya uamuzi wenu wa kunipeleka shuleni hayawezi kutoshea hata chapisho la kurasa elfu.

Si kudhihakiwa na miale ya jua; ngozi yangu inashindwa kuuhimili ukali wake, si kutengwa na marika, si kulazimika kusoma hati za kawaida hadi pale serikali ilipoanzisha sera ya kuhakikisha kwamba matini zote za kiusomi zimeandikwa pia kwa hati ambazo zinaweza kusomwa na Wenye changamoto kama yangu, si kubaguliwa kazini….”

Bahati alitua, akawatazama wazazi wake kama anayetaka kuona taathira ya maneno yake kisha akaendalea.

“Msinione kama aliyckosa hisani, ila’ nataka niwaambie kwamba hata uamuzi wenu wa kunitafutia mlinzi kuandamana nami hadi shuleni ulinitia kwenye ngome zaidi.

Nilijihisi kama niliyedhulumiwa zaidi katika kule kulindwa! Najua mlikuwa mnachelea kwamba ningekuwa windo rahisi kwa walanguzi wa binadamu ambao wanaamini kwamba viungo vyetu sisi ni dawa ya kutibia ndwele mbalimbali.

Hata hivyo, katika kipindi chote hicho nilitamani kwamba mngcnifimza mbinu za kujilinda mimi binafsi. Amini usiamini hata nilitamani kwamba ningetekwa nyara, nijadiliane na Watesi wangu kuliko kupokwa nafasi ya kubuni mikakati ya kujihakikishia usalama”.

“Mwanangu Bahati,” alisema mume wangu, “binadamu hawi jagina kwa kuzifimta tamaduni za jamii yake bila kuzichunguza. :haidhuru kwamba ilichukua muda kuyangamua haya’. La muhimu ni kwamba umeweza kuishi kama ndugu zako”.

Nilimtazama mume wangu kwa macho yaliyokuwa yamepofushwa na dimbwi la machozi. Moyo uliituma akili yangu kurudi nyuma kule -e-e-e- kwenye miereka ya baada ya kuzaliwa kwa Bahati. Asubuhi hiyo ya kipupwe nilishika ujia ulioelekea kwenye msitu uliokuwa karibu na boma la Mzee Kedi, baba mkwe wangu; mgongoni nimeifungia mbeleko ambayo ilikisitiri kitoto changu. Nilitazama nyuma, nikaiona nyumba ambayo mimi na mume wangu tulikuwa tumechanga bia kuijenga.

“Haya yote nayaacha,” nilijiambia, “nayaacha na mengine mengi. Nawaacha mabinti wangu wawili, namwacha mume wangu, naiacha kazi yangu, nayaacha rnaisha yangm Wala sijuti kwa kuyaacha haya yote. Sina cha kujutia kwani imebidi kuondoka. Jamii yangu imenitema; mimi na mwanangu.

Haina nafasi ya mwanangu, kwa hivyo nami nimeamua kwamba haina nafasi yangu kwa vile imesema huu ni mzigo wangu. Ikiwa ukoo umeamua kuwa hatima ya mwanangu huyu ni kuwa kitoweo cha fisi, basi na tuwe sote karamu ya fisi,” nilitamatisha kauli yangu kisha nikayarudisha nyuma tena mawazo yangu.

Nilikumbuka sauti ya muuguzi hospitalini siku ambayo nilijikopoa, “Pongezi Tamasha, Mungu amekutunukia kipusa”. Nilikifunua kitoto changu kilichokuwa kimefunikwa gubigubi, nikakitazama viguu, vikono, uso…kisha, ‘Mungu wangu!’ ikanitoka. “Dadangu, unastahili kumshukuru Mungu,” akasema rnuuguzi, “wapo wanawake, mimi mwenycwe nikiwemo, ambao hawajawahi kuambulia uj auzito, sikwambii hata kupoteza mimba.

Huyu wako ni kiumbe kamili, kasoro yake i kwenye ngozi tu, na hii ni hali ambayo unaweza kukabiliana nayo. Hapa lmionapo nimelazimika kumpa mume wangu talaka, mwenyewe alienda kortini akaiomba. Anadai kwamba hatusikilizani. Ila najua kiini cha haya yote ni kutoshika kizazi”.

Nilimtazama huyo muuguzi kana kwamba hajaserna lolote. Nilimwona kama anayeuona mzigo wangu kuwa kanda la usufi. Huenda huyu muuguzi hakujua kwamba katika jamii yangu watoto wa aina hii ni kama pacha, huaminiwa kuwa nuksi kwa ukoo mzima, kwa hivyo hutupwa. Muuguzi huyu hakujua pia kwamba tayari nilikuwa na watoto wawili wa kike na huo tayari ulikuwa mzigo mkubwa kwaugu kwani ilibidi kumhakikishia mavyaa kila mara kwamba hawa pia walikuwa watoto.

Moyo ulinipa kukumbuka jitimai iliyojiandika usoni mwa mume wangu asubuhi hiyo alipokuja hospitalini. Alikitamma lcitoto chetu kana kwamba anaona mzuka. Alinyamaza kwa muda, akashusha pumzi, kisha akanishika kwenye bega na kuondoka kwenyc wodi. Machozi yalivunja kingo zake huko yanakohifiadhivya, nikalia kama mfiwa, Mume wangu alirudi tena baada ya siku mbili; anakuja kunipcleka nyumbani.

“Mke wangu, naomba msamaha kwa kutokuja kuwatazama kwa siku mbili. Ilibidi nishauriane 11a ukoo kuhusu lnnzia Inavyoonekana ni kwamba msimamo wa baba na wazee wenginc ni ule ule. Wanasema ukoo wa Baulanga haujawahi kupata mtoto wa aina hii, kwarnba kumhifadhi mwana huyu kumkuwa kuupaka masizi ukoo. Wahenga hawatakubali tendo hili. Sijui nitakutetea vipi.

Nimo kwenye njia panda,” mume wangu alikamlisha uzungumzi wake na kuelekea kwenye afisi ya mhasflm kukamilisha w’viga vya kutuondoa hospitalinj. “Huna haja ya klmitetea. Sijafanya kosa lolote. Nililofanya ni kujaliwa kiumbe ambaye anaonekana kuwa punguani kwa misingi ya jamii yako. Nitakilinda kitoto hiki hata kifoni,” nilimwambia mume wangu mawazoni.

(a) “Kufauikiwa kwa watu wenye mahitaji maalumu ktmategemea jamii.” Thibitisha kwa kutoa hoja sita kutoka aya tatu za kwanza. (alama 6)

READ ALSO:  KCSE Business Studies Paper 1 2019 PDF: Free Past Papers

(b) Kwa kurejelea aya ya nne hadi ya saba, onyesha jinsi unyanyasaji Wa kijinsia unavyoendelezwa katika jamii hii. (alama 3)

(c) “Msimulizi anahimiza. uwajibikaji.” Thibitisha kwa kutoa hoja nne kutoka aya tatu za ‘ mwisho. (alama 4)

(d) (i) Andika kisawe cha, ‘hisani’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 1)

(ii) Elcza maana ya, ‘kuupaka masizi’ kulingana na taarifa. (alama 1)

2. UFUPISHO: (Alama 15)

Soma kifimgu kifitatacho kisha ujibu maswali.

Moja kati ya mambo ambayo yarnerahisisha maisha ya binadamu ni maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia. Siku hizi shughuli nyingi ambazo zilichukua muda kutekelezwa zinachukua muda mfupi sana. Tuchukue kwa mfano shughuli za usafiri na utendaji kazi.

Siku hizi zipo mashinc ambazo zinafanya kazi kuwa nyepesi mno. Kwa mfano, katika ukulima, kuna mashine za kulima, kuvuna na hata kupura nafaka.

Magari nayo yamerahisisha usafili na upashanaji habari. Safari ambayo awali ilichukua siku mbili au tam, siku hizi inachukua siku moja an hata saa chache tu kwa sababu ya kuwepo kwa magari ya kisasa.

Katika sekta ya elimu, maendeleo makubwa yameshuhudiwa. Siku hizi mwalimu anaweza kuhuisha some lake kwa kutumia. tarakilishi. Vipindi mbalimbali vimenaswa na kuhifahiwa kwenye kompyuta.

Itokeapo kwamba mwalimu wa darasa atakosa kuhudhurj/a somo, wanafunzi wanaweza kufunzwa na mwalimu wa kompyuta. Shughuli za utafiti nazo zirnefaidika mno kutokana na uvumbuzi wa kiteknolojia. Wasomi na wanafunzi wanaweza kupata matini mbalimbali za rejea kupitia kwenyc mtandao. Hili linasaidia kufidia upungufu Wa vitabu vya kikaida.

Hali kadhalika, maendeleo ya kiteknolojia yamerahisisha shughuli za usajili vyuoni na hata shuleni. Wanafimzi wanaweza kujisajili na hata kulipia kozi mbalimbali kupitia kwenye mtandao. Hali hii inaokoa muda ambao watahiniwa na wanaafunzi wangepanga foleni vyupni, na hata katika taasisi zinazotoa mitihani, ili kujisajili. Kadhalika, teknolojia imcsaidia katika kuhakikisha usalama wa alama za wanafunzi. Wataalarnu Wa teknolojia wameweza kuweka mikakati ambayo itahakikisha kwamba mabadiliko yoyote ya alama yanaweza kufuatiliwa kupitia kwenye mtandao.

Upande Wa matibabu nao haujaachwa nyuma. Utafiti kuhusu tiba za kukabiliana na magonjwa sugu unafanywa kupitia kwenye mtandao wa intaneti. Pia, kuna mitambo ya kuchunguzia viini vya magonjwa mbalimbali na kutoa matokeo hapo hapo.

Hali hii husaidia kumpa mgonjwa matibabu yafaayo Wakati ufaao, hivyo kuokoa maisha yake. Madaktari pia wanaweza kufanya udodosi hapo hapo kwa kubofya tu tarakilishi.

Yumkini manufaa zaidi ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yamepatikana kwenye uwanja Wa biashara na uchumi kw; jumla. Ni dhahiri kwamba siku hizi ubadilishanaji wa bidhaa na huduma umekuwa rahisi mno. Kwa mfan0,- mfanyabiashara anaweza kuuza na kununua bidhaa zake kutoka nga’mb0 akiwa hapo hapo kiwandani au afisini mwake. Hali hii imefanikishwa hata zaidi na uvumbuzi wa simutamba; kifaa kidogo lakini chenye akili kama ya bindarnu.

Kifaa hiki huwa na huduma ya intaneti ambayo humwezcsha muuzaji kumtumia mnunuzi picha ya bidhaa aitakayo akiwa popote pale. Kifaa hiki pia ni muhimu katika kuendeleza huduma za benki. Je, unajua kwamba unawczz kutoa na kuhifadhi fedha kwenye akaunti yako kwa sekunde mbili au tatu ukiwa hapo hapo sebuleni mwako? Unajua pia unaweza hata kuomba na kupokea mkopo kupitia simu yakq ya mkqnoni? Huduma hii ya sirnutarnba pia humwezesha mtu kuwatumia pesa jamaa zakc bila kulazimika kwenda benki au posta kuzituma.

Mtu anaweza hata kuhifadhi laki moja kwenye simu na kuzituma pesa hizo kulingana na matilaba yake. Kadhalika mtu anaweza kulipia huduma kama vile za umeme, maji, matibabu na hata karo kupitia kifaa hicho hicho. Ni dhahiri kwamba uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia umeiletea jamii natija kubwa.

Hata hivyo, halqma mchele usiokuwa na ndume.

Macndeleo haya yameandamana na changamoto anuwai. Kuwepo kwa mtandao wa intaneti kumewafanya baadhi ya wanaj amii kutumia muda wao mwingi kwenye mtandao, mara nyingine kwa nia ya kujiburudisha tu au kuzungumza na marafiki.

Hili linapalilia kuzorota kwa maadili ya kikazi. Aidha, kuna baadhi ya watu arnbao wanatumia mtandao kuwatusi na lcuwadhalilisha wengine kwa namna mbalimbali.

Wengine huingilia uhuru wa kibinafsi wa wenzao kwa kuangaza mahusiano yao ya kimapenzi. Hali kadhalika, kuna wanajamii ambao hutumia mtandao kuwatisha wengine. Baadhi hutumia mtandao kuwatapeli wengine.

Pengine hata wewe urnewahi kupigiwa simu ukaambiwa umeshinda milioni moja, ukaanguka kwenye mtego huo, na baadaye hata ukapoteza kiasi fulani cha fedha ukifuata milioni ambayo haipo! _ Uvumbuzi wa kiteknolojia umechangia kuendeleza wizi wa kitaaluma. Kuna wasomi katika ngazi mbalimbali atnbao hunakili mawazo ya wataalamu moja kwa moja bila hata kutambua mchango wao kwenye marejeleo.

Hii ni njia moja ya kudhoofisha fani yenyewe ya utafiti. Kadhalika, mtandao wa intaneti umetumiwa na watu Waliopotoka kimaadili kupujua thamani ya mtihani. Baadhi ya watu huchukua sehemu ya mtihani au hata karatasi nzima ya mtihani wakaipiga picha na kuituma kwa wateja wao kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Visa vya kigaidi navyo vinaendelezwa kwa ufanifu mkubwa kupitia kwenye mtandao Wa intanenti na simu za Inkononi. Njama nyingi za ulipuaji Wa majengo zimepangwa kupitia simutamba.

Vilevile, uvumbuzi Wa kiteknolojia unatishia kutetercsha mshikamano Wa kifamilia. Siku hizi mzazi anaweza kukaa kwa miezi miwili bila kuonana ana kwa ana na watoto wake, wanazungumza tu kupitia kwenye simu.

Hili hutepua ule uhusiano wa kibinafsi kati ya jamaa, na mwishowe huweza kusababisha ukengeushi; watoto na wazazi wakajiona kuwa Wageni kwa kila mmoja Juu ya hayo, huduma zinazopatikana kwenye mtandao zimewafanya vijana kuwa waraibu kiasi cha kutotenga wakati kuyadurusu masomo yao. Hili linawatia kiwewe wakati wa mtihani na yumkini ni mojawapo ya vyanzo vya udanganyifu katika mitihani.

Maendcleo ya kiteknolojia yamesaidia kuimarisha maisha ya binadamu katika nyanja zote za maisha. Binadamu wameweza hata kupata mafundisho ya kidini moj a kwa rnoja kupitia kwenye simu zao za mkononi.

Hata hivyo, binadamu ameweza pia kuhasirika kutokana na uvumbuzi huu. Mashine zimetwaa nafasi ya binadamu katika utendakazi, jambo ambalo linapalilia zaidi uhaba wa nafsi za kazi. Ni muhimu binadamu ajitahidi kutumia teknolojia kwa njia endelevu ili kujifaidi.

(a) Fupisha ujumbe wa aya nne za kwanza kwa maneno 90. (alama 8, 1 ya rntiririko) Matayarisho Nakala Safi (b) Fafanua masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (maneno 70) (alama 7, 1 ya mtiririko) Matayarisho

………………………………………………

……………………………………………….

……………………………………………….

………………………………………………..

Nakalasafi

…………………………………,…………….

……………………………………………….

………………………………………………..

…………………………………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)

(a) Andika tofauti moja kati ya sauti zifuatazo: (alama 2)

(i) /ng’/na/gh//

(ii) /v/ na /f/

(iii) /r/na/l/

(iv) /m/na/n/

(b) Andika.

(i) konsonanti, konsonanti, konsonanti, irabu, konsonanti, irabu

(ii)konsonanti, konsonanti, irabu, konsonanti, irabu

(c) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mbili ya kiambishi O

(d) Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo. (alama‘2)

(i) Mhalifu alisamehewa kwa sababu alinyenyekea.

(Geuza maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino.)

(ii) Waigizaji wengine wameingia jukwaani.

READ ALSO:  KCSE History Paper 2 2014 PDF: Free KNEC Past Papers

(Tumia kivumishi cha idadi chenye kuonyesha nafasi katika orodha.)

(e) Tunga sentcnsi ukirumia kirai kihusishi kama kielezi.

(f) Unganisha sentensi zifuatazo kwa viunganishi mwafaka.

(i) Kheri aliweza kutuj engea hospitali. Ataj cnga zahanati pia.

(ii) Zumari anasomea unawsheria vile vile Maki anasomea unasheria

(g) Onyesha miundo ya nomino kafiika ngeli ya A — WA.

(h) Tunga sentensi katika wakati uliopo hali isiyodhihirika.

(i) Andika sentensi ifuatayo katika umoja.

‘ Maseremala walilainisha mbao hizo wakatutengcnezea meza.

(j) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.

. (i) Kaumu amewafanya mifugo wangu wanywe maji.

(Anza kwa: Mifugo wangu , usitumie, ‘amewafanya’.) (ii) Wanakijiji wanaishi karibu na msitu. Wanakijij i hawawavamii wanyama.

(Ungamsha kuunda sentensi ambatano.)

(k) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.

Ngoma hizo zao ziliibwa na wezi Wale.

(I)Tumia ‘kwa’ katika sentensi kuonyesha:

(i) schemu ya kitu kizima (alama 1)

(ii) namna tendo lilivyofanyika (alama 1)

Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. (alama 2)

“Kusoma kwa mapana kutapalilia ubunifu wa wanafunzi hawa wenu,” mtaalamu akatuambia.

Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)

Vlwanda vikianzishwa masharnbani idadi ya wanaohamia mjini itapunguzwa.

Tunga sentensi zenye miundo ifuatayo. (alama 2′)

(i) KN(N+RH)+KT(Ts+’l’)

(ii) KN(V+N)+KT (t+v)

Ainisha yambwa katika sentensi ifuatayo.

Mhunzi alimfulia rnjukuu wake pete ya shaba. (alama I)

Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo.

Bedui alimrushia tufe. _

Alama za mtajo hutumiwa kufungia maneno halisi ya msemaji. Tunga sentensi ml kuonyesha matumizi rnengine mawili ya alama za mtajo.

(s) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kutumia kinyumc cha mancno yaliyopigiwa mstari Mwanafimm mkakamavu huzingatia masomo yake. (

(t) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya rithi na ridhi.

(u) Tunatumia similc tunapotaka mtu atupishe, …. ..tunapoomba kitu kinusurike, na kefule……… ……………………….najambo, (alama 1)

(v) Andika visawe vya mancno yafuatayo:

(i) doa

(w) Andika sentensi ifuatayo upya kulingana na rnaagizo.

Maneo haya yana uyoga

(Anza kwa: Uyoga.)

4. ISIMUJAMII: (Alama 10)

Soma makala yafizatayo kisha ujibu maswali.

“Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, mahakama hii irnethibitisha bila chembe ya shaka kwamba wewe mshtakiwa, Bi Mlachake Chauchau ndiye uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha vifo vya raia harnsini na kupofuka kwa wengine mia moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji.”

(a) Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa rnifano miwili kutoka kwenyc makala. (alama 2)

(b) Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo zingejitokeza katika makala haya. (alama 8) ’

KCSE Kiswahili Paper 2 2017 Questions and Answers

KCSE Kiswahili Marking schemes Paper 2 2017

Kiswahili and Government paper 2

Lugha

Ufahamu Maswali na Majibu: (Alama 15)

(a) “Kufauikiwa kwa watu wenye mahitaji maalumu ktmategemea jamii.” Thibitisha kwa kutoa hoja sita kutoka aya tatu za kwanza. (alama 6)

 

 • Wazazi Wanampeleka Bahati shuleni.
 • Bahati kupata dhiki ya kisaikolojia kwa kudhihakiwa
 • Wazazi kumtafutiaB ahati mlinzi wa kumkinga na wateka nyara.
 • Bahati na wengine kama yeye kusoma hati za kawaida hapo awali
 • Bahati kubaguliwa kazini
 • Serikali kuhakikisha matini zimeandikwa kwa hati inayoweza kusomwa na Walemavu
 • Wazazi hawamfunzi Bahati mbinu za kujilinda, hivyo anajihisi mfungwa.
 • Walanguzi Wa Watu kuhatarisha usalama wa watoto wa aina ya Bahati
 • Ukoo kuamua kuangamiza watoto wenye ulemavu
 • Bahati kudhihakiwa shuleni/kutengwa na Wenzake
 • Mama/wazazi kuamua kumhifadhi Bahati Tanbihi Mtahiniwa anaweza kuangazia dhuluma pekec. Anaweza pia kuangazia utekelezaji wa haki kwa Watu Wenye mahitaji maalumu pekee. Anaweza pia kuchanganya hoja. Mradi amedondoa hoja sita. ((b) Kwa kurejelea aya ya nne hadi ya saba, onyesha jinsi unyanyasaji Wa kijinsia unavyoendelezwa katika jamii hii. (alama 3)

  (i). Muuguzi kutalikiwa kwa kutopata mtoto

  (ii). Watoto Wa kike kuonekana kuwa mzigo/si Watoto

  (iii). Kusimangwa na mavyzia — kuwa hajazaa Watoto.

  (c) “Msimulizi anahimiza. uwajibikaji.” Thibitisha kwa kutoa hoja nne kutoka aya tatu za ‘ mwisho. (alama 4)

 • Mume kuondoka bila neno kwa mkewe ~ anakuja kuomba msamaha.
 • hisia za mama/wazazi
 • Mume kumjuza mke uamuzi wa ukoo
 • Mume kulipia gharama ya matibabu
 • Msimulizi kuamua kukihifadhi kitoto chake
 • Msimulizi anakashifu mtazamo Wa jamii kuhusu watoto wa aina hii. (aya ya mwisho) ‘ Tanbihi Mtahiniwa anaweza kuonyesha uwajibikaji au hata ukosefu Wa uwajibikaji. Anaweza kuchanganya hoja pia.(d) (i) Andika kisawe cha, ‘hisani’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 1)
 • Hisani- fadhila, shukrani (alama 1)(ii) Eleza maana ya, ‘kuupaka masizi’ kulingana na taarifa. (alama 1)
 • Kuupaka masizi — kuuharibia sifa/ kuuaibisha2. Ufupisho Maswali na Majibu: (Alama 15)

  (a) Fupisha ujumbe wa aya nne za kwanza kwa maneno 90. (alama 8, 1 ya mtiririko) Matayarisho

  Sayansi na teknolojia zimerahisisha maisha ya binadamu.

 • Mashine zimerahisisha utenda kazi.
 • Mtu anaweza kusomesha hata bila kuwepo.
 • Kuimarisha shughuli za utafiti
 • Kurahisisha usajili Wa wanafunzi na watahiniwa vii. Kuimarisha matibabu kupitia utafiti
 • Kufanya udososi hapo hapo
 • Kurahisisha ubadilishanaji bidhaa
 • Kuhifadhi na kutuma pesa
 • Kulipia huduma(b) Fafanua masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (maneno 70) (alama 7, 1 ya mtiririko) Nakalasafi

  .

 • Nafasi ya uvumbuzi wa kisayansi
 • Kuzorotesha utenda kazi
 • Kuingilia uhuru Wa kibinafsi
 • Kuwatisha wengine
 • Kuwamsi na kuwadhalilisha wengine
 • Kuwatapeli vii. Wizi Wa kitaaluma vm. Upujufu Wa thamani ya n1tihani/ Wizi Wa mitihani
 • Visa vya kigaidi kuendelezwa kupitia mtandao
 • Kumomonyoa mshikamano wa kifamilia- mawasiliano ya sirnu badala ya ana kwa ana
 • Vijana kupuuza masomo kwa kuwa Waraibu wa mtandao
 • Binadamu huweza kupata mafundisho ya kidini kupitia mtandao.
 • Kupalilia ukosefu wa ajira
 • Binadamu atumie teknolojia kwa njia endelevu ili kujifaidi.3. MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)

  (a) Andika tofauti moja kati ya sauti zifuatazo: (alama 2)

  (i) /ng’/na/gh/-- /ng’/ni nazali na /gh/ni kikwamizo

  (ii) /v/ na /f/-- /v/ ni ghuna na /f/ sighuna.

  (iii) /r/na/l/-- /r/ ni kimadende na /l/ ni kitarnbaza.

  (iv) /m/na/n/-- /m/ hutamkiwa midomoni i1hali/n/ ni ya ufizi.

  (b) Andika.

  (i) konsonanti, konsonanti, konsonanti, irabu, konsonanti, irabu

  mfano:mbweha, ngwena, ndwele

  (ii)konsonanti, konsonanti, irabu, konsonanti, irabu

  mfano:ndama, mkate, ngama, ndizi, mkeka

  (c) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mbili ya kiambishi O

 • Kirej eshi cha nafsi ya tatu wingi — Wafanyakazi walioajiriwa wana bidii.
 • Kirejeshi cha ngeli ya U — I — Umoja Mgiu uliotibiwa umepona.
 • Kirejeshi cha ngeli ya U — ZI — umoja Ufa uliozibwa ni huu,
 • Kirejeshi cha ngeli ya U — YA — umoja Ugonjwa huu ndio uliotibiwa.
 • Kirejcshi cha ngeli ya U — U — Wema aliomonyesha ulituvutia.
 • Kuonyesha tokeo la kitu/kuonyesha nomino/unominishaji(d) Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo. (alama‘2)

  (i) Mhalifu alisamehewa kwa sababu alinyenyekea.

  (Geuza maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino.)

  -- Mhalifu alipata (alipewa) msamaha kwa sababu (kwa) unyenyekevu wake.

  (ii) Waigizaji wengine wameingia jukwaani.

  (Tumia kivumishi cha idadi chenye kuonyesha nafasi katika orodha.)

  -- Waigizaji wa kwanza/wa mwisho wameingia ju.kwaani

  (e) Tunga sentensi ukitumia kirai kihusishi kama kielezi.

  (i)Mama huyo aliwapenda wanawe kwa dhati.

  ii. Bendera ilikuwa juu ya mlingoti.

  (iii). Mkurugenzi aliwasili kabla ya mkutano kuanza.

  iv. Kaire ni mrefu kuliko baba yake.

  (f) Unganisha sentensi zifuatazo kwa viunganishi mwafaka.

  (i) Kheri aliweza kutujengea hospitali. Atajenga zahanati pia.

  -- Kheri aliweza kutujengea hospitali sembuse zahanati!

  (ii) Zumari anasomea unasheria vile vile Maki anasomea unasheria

  -- Zumari na Maki wanasomea Uanasheria.

  (g) Onyesha miundo ya nomino kafiika ngeli ya A — WA.

  Nomino zinazoanza kwa ‘m’ katika umoja na ‘Wa’ katika wingi. Mfano: Mbunge ~ Wabunge

  ii. Zinazoanza kwa mw katika umoja na wa katika wingi.

  Mfano Mwanasheria ~ Wanasheria j n m. Nomino za pekee zinazotaja watu. Maria ametutembelea.

  iv. Zinazoanza kwa’ki’ katika umoja na‘vy’ katika wingi

  a) Kijana huyu ameheshimika. Vijana hawa wameheshimika.

  b) Kiboko angalimajini. Viboko wangali majini.

  v. Ambazo hazina mianzo maalum ila huchukua viambishi A — WA vya upatanisho wa kisarufi.

  Kwa mfano, simba, kuku, bata, mama, baba. Simba huyu amehifadhiwa. Simba hawa wamehifadhiwa.

  (h) Tunga sentensi katika wakati uliopo hali isiyodhihirika.

  (i) Wanariadha Wacheza uwanj ani.

  ii. Jua lachomoza asubuhi.

  iii. Sisi twasoma vitabu.

  iv. Mwalimu afundisha darasani.

  (i) Andika sentensi ifuatayo katika umoja.

  ‘ Maseremala walilainisha mbao hizo wakatutengenezea meza.

  -- Seremala alilainisha ubao huo akanitengenezea meza.

  (j) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.

  . (i) Kaumu amewafanya mifugo wangu wanywe maji.

  (Anza kwa: Mifugo wangu , usitumie, ‘amewafanya’.) Mifugo wangu wamenyweshwa maji na Kaumu.

  (ii) Wanakijiji wanaishi karibu na msitu. Wanakijiji hawawavamii wanyama.

  (Ungamsha kuunda sentensi ambatano.)

  Wanakijiji wanaishi karibu na misitu lakini|ila|bali|i1hali hawawavamii wanyama

  (k) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.

  Ngoma hizo zao ziliibwa na wezi Wale.

  Magoma hayo yao yaliibwa na majizi yale.

  (I)Tumia ‘kwa’ katika sentensi kuonyesha:

  (i) schemu ya kitu kizima (alama 1)

  Watoto Watatu kwa kumi hupata chanjo hiyo

  (ii) namna tendo lilivyofanyika (alama 1)

  Wengine walipata tisa kwa kumi katika tamrini hiyo.Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. (alama 2)

  “Kusoma kwa mapana kutapalilia ubunifu wa wanafunzi hawa wenu,” mtaalamu akatuambia.

  -- Mtaalamu alituambia kwamba kusoma kwa mapana kungepalilia ubunifu wa wanafunzi haowetu

  Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)

  Viwanda vikianzishwa masharnbani idadi ya wanaohamia mjini itapunguzwa.

  (i)Viwanda vikianzishwa mashambani — kishazi kitegemezi

  (ii) Idadi ya wanaohamia jijini- kishazi kitegemezi

  (iii) Itapunguzwa — kishazi huru

  Tunga sentensi zenye miundo ifuatayo. (alama 2′)

  (i) KN(N+RH)+KT(Ts+’l’)

  -- Umati wa Watu ulikuwa ukimshangilia.

  -- Kisu cha baba kinahitaji kunolewa

  (ii) KN(V+N)+KT (t+v)

  -- Mwenye duka angali mwaminifu. b) Yule dalali alikuwa shupavu

  Ainisha yambwa katika sentensi ifuatayo.

  Mhunzi alimfulia mjukuu wake pete ya shaba. (alama I)

  Mjukuu wake — yambwa tendewa (kitondo) Pete ya shaba -- yambwa tendwa (kipozi) Tanbihi

  Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo.

  Bedui alimrushia tufe.

  (i)Alirusha tufe kwa niaba ya mhusika huyo.

  (ii) Alirusha tufe kuelekea kwa mhusika huyo.

  (iii) Alirusha tufe ya mhusika huyo.

  (iv) Alimrusha mhusika huyo kwa sababu ya tufe.

  Alama za mtajo hutumiwa kufungia maneno halisi ya msemaji. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mengine mawili ya alama za mtajo.

  (i)Kufungia neno la kigeni- “mukimo”

  (ii) Kuonyesha neno lina maana nyingine na unayomaanisha, k.m. binamu kumaanisha ‘mpenzi’.

  (iii) Kufungia anwani- “Pendo la Karaha”

  (iv) Kuonyesha neno halij akubaliwa katika lugha unayoandikia/unayoziingumza.

  (s) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kutumia kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari Mwanafunzi mkakamavu huzingatia masomo yake.

  -- Mkakamavu — mzembe/mvivu/mnyonge/goigoi/Intepetevu/dhaifu huzingatia masomo yake

  (t) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya rithi na ridhi.

  -- Rithi — kupata mali/maarifa au ujuzi kutoka kwa mtu/makala fulani Ridhi — kukubali au kupendezwa na jambo/kutoa ruhusa jambo litendeke.

  (u) Tunatumia simile tunapotaka mtu atupishe, hamadi..tunapoomba kitu kinusurike, na kefule……..tunapoudhika. …tunapokasirishwa……….na jambo,

  (v) Andika visawe vya maneno yafuatayo:

  (i) doa

  -- dosari, kosa, hitilafu, ila, baka

  (ii)omba — rai, sihi, sali

  (w) Andika sentensi ifuatayo upya kulingana na maagizo.

  Maneo haya yana uyoga

  (Anza kwa: Uyoga.)

  (i) Uyoga hupatikana kwenye maeneo haya.

  ii) Uyoga hupatikana katika maeneo haya.

  iii) Uyoga upo kwenye maeneo haya.

  4. ISIMUJAMII: (Alama 10)

  Soma makala yafizatayo kisha ujibu maswali.

  “Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, mahakama hii irnethibitisha bila chembe ya shaka kwamba wewe mshtakiwa, Bi Mlachake Chauchau ndiye uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha vifo vya raia harnsini na kupofuka kwa wengine mia moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji.”

  (a) Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa rnifano miwili kutoka kwenyc makala.

  -- Sajili ya mahakamani/sajili ya kisheria

  i) Matumizi ya sentensi ndefu -- sentensi ya kwanza inatakriban maneno 30.

  (ii) Msamiati maalum Wa kisheria kama vile ‘ushahidi’,‘mahakama’,‘unahukumiWa’

  (iii) Kuzungumza na mshukiwa moja kwa m0ja- wewe mshukiwa

  (iv) Kutoa hukumu

  (b) Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo zingejitokeza katika makala haya. (alama 8)

  (i) Matumizi ya lugha chakavu/kikale

  (ii) Kunukuu vifungu vya sheria ili kuondoa shaka.

  (v) Kuzingatia urasmi kwa kiasi kikubwa

  (vi) Urudiaji unaonuiwa kuweka wazo wazi/kusisitiza

  (vii) Msamiati Wa kawaida hupcwa/huwa na maana maalum. Kwa mfano unaposema, “Leamed Friend”, kurnaanisha mwanasheria.

  (viii) Lugha ya kuhoji/kudadisi, hasa pale mshukiwa/shahidi anapohojiwa.

  (ix) Sheria za kisarufi huzingatiwa kwa kiasi kikubwa ili kukinga dhidi ya kupotosha maana.

  (X) Wakati mwingine sheria hizi huweza kuvunjwa ili kukidhi haja ya mawasiliano, hasa pale mshukiwa hajasoma/haelewi lugha rasmi au lugha sanifu.

  (xi) Kauli fupifupi hasa wakati wa kuhoji.

  (xii) Upashanaji zamu kwa kawaida hudhibitiwa na kiongozi wa mashtaka.

  (xiii) Kuchanganya au kubadilisha msimbo huweza kutokea.

  (xiv) Lugha ya kushawishi, hasa pale wakili anapotoa utetezi

  (xv) Toni kali pale hakimu anapotoa hukumu.

 

 

If You want the marking schemes, send Us an email at: smartjohnene@gmail.com indicating your the subject and your name and We will guide You on How to get the documents.

KCSE Kiswahili Paper 1 2017

->> Click Here to download Kiswahili KCSE Paper 1 2017 PDF

KCSE Kiswahili Paper 3 2017

->> The KCSE Kiswahili Paper 3 2017 exams are yet to be available soon

After a successful purchase of the past Papers It is time for revision. Put in your best and get the best out of your KCSE Exams.

To purchase the Comprehensive KCSE KCSE Kiswahili Paper 2 2017 PDF, Go to the Matric Exam Papers Master Page

KCSE Kiswahili Paper 2 2017 Navigation Panel:

We guess this information on KCSE Kiswahili Paper 2 2017 PDF was really helpful, tell Us What You think in the comment session below. We wish to hear your views, do not forget to use the share buttons below to share with others.

READ ALSO:  KCSE English Paper 1 2017: Review Free Past Papers PDF
       

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.